Goma: Mwanabunge Alexis Bahunga asema kwamba DRC ni ya wakongomani wote ila siyo watu wamoja peke

Mwanabunge Alexis Bahunga mcaguliwa wilayani Masisi Kivu ya kaskazini

Alexis Kahunga mcaguliwa wa Masisi amerudi hii ijumaa mjini Goma toka Kinshasa ambako alishiriki kwenyi kikao kilichoandaliwa na chama cha kisiasa Ensemble pour la Republique kwa mwito wake Prezidenti Moîse Katumbi TCHAPWE.

Mwanabunge huyu anena mbele ya wandishi habari kwamba Moise Katumbi angojea maoni ya wafwasi wake na hata raia kwa jumla ili kutangaza rasmi musimamo wao, kuendelea kujiunga na Muungano Union sacrée ama la.

Akilinganisha DRC na meli ambayo Kiongozi hajue nafasi ya kuelekea.

DRC yafananishwa na meli kwenyi ziwa ambayo mwendeshaji hajuwe aelekeye upande gani. Ndiyo maana wasafiri walio ndani wapashwa moja kwa moja kujitupa upande wake ili kujiokowa » anena Alexy Bahunga.

Mwanabunge alijibu kwa maswala mengine akionyesha kuwa hali yazorota kiusalama, kijamii, kimaendeleo na kadhalika. Na kwamba hali iliweza zorota tangu uongozi wake Joseph Kabila na hadi sasa hakuna kilicho badilika, aongeza Mwanabunge Alexy Bahunga Malira mcaguliwa wa Masisi.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire