Goma: Patrick MUNDEKE anena kwamba Prezidenti wa chama chake Moise KATUMBI aheshimu sheria kwa manufaa ya raia

Patrick MUNDEKE Mshauri ahusikae na maswala ya vijana wake Moïse KATUMBI

Akihojiwa na wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma nne tarehe 9 novembre 2021, mshauri husika na maswala ya vijana wake Moïse KATUMBI atoa kwanza ujumbe wa hongera toka kwake Moise KATUMBI kwa raia wenyi kukumbwa na vita pa Kanyabayonga, Kibumba na penginepo jimboni Kivu ya kaskazini.

Patrick MUNDEKE anena kuwa Prezidenti wa chama cha kisiasa » Ensemble pour la République » Moise KATUMBI kwa ushirikiano na vyama vingine vya kisiasa alikutana na uratibu wa chama hicho toka majimbo ili kuchunguza sheria kuhusu chama chao na hii itapelekea kuchukua hatua ya kubaki ndani ya Muungano Union sacrée ama la. Kwa kuwa hali ya maisha ya raia yazorota siku kwa siku .

Patrick Mundeke aendelea kwamba Moise Katumbi ni mheshimu wa katiba kwa manufaa ya raia.

Mshauri ahusikae na maswala ya vijana wake Moise Katumbi aona umuhimu wa kuandaa kikao ili kuzungumza kuhusu matatizo yenye kukumba DRC.

« Ingelikuwa heri Raisi wa DRC Félix Antoine TSHiSEKEDI kuandaa kikao kitakacho kusanya wakongomani toka pande zote mfano wa kongamano ya mwaka 2009 iliyofanyika mjini Goma. Humu tutazungumza shida chungu télé zenyi kukwamisha maendeleo ya DRC na kutafuta suluhu ya pamoja. Kuongoza siyo kujipiga kifua ni kukaa na kuzungumza pamoja ili kutafuta suluhu. Inaonekana hadi sasa kwamba uongozi wa kijeshi haufaulu .Inabidi kutekeleza usalama mashariki mwa DRC. Ndio maana pamoja kutafuta suluhu kama wakongomani  » aeleza Patrick Mundeke mbele ya wandishi habari.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire