Goma: Robert Seninga anena kukutana na Prezidenti wa seneti mjini Kinshasa kuhusu usalama jimboni mwake

Prezidenti wa bunge la Kivu ya kaskazini akitokea mjini Kinshasa

Akiwasili hii ijumaa tarehe 26 novemba kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma, Prezidenti wa bunge la jimbo la Kivu ya kaskazini Robert Seninga anena kukutana na viongozi kadhaa wa DRC hususan Prezidenti wa bunge la taifa kuhusu usalama mdogo mashariki mwa DRC kwa upeke na jimboni Kivu ya kaskazini kwa jumla.

Huyu alipokelewa naye Adele Bazizane mwandishi kwenyi bunge la jimbo la Kivu ya kaskazini mbele ya wapasha habari.

« Tulipokelewa na Prezidenti wa seneti ,namna ya uhusiano kati ya bunge za majimbo na seneti kulingana na katiba ya nchi. Wana seneti wakiwakilisha majimbo wana mhula wa miaka mitano jisi inavyo fahamika. Pamoja na shirika za serkali tulinena kufanya iwezekanayo ili kutekeleza maendeleo ya majimbo « aeleza Prezidenti wa bunge Robert Seninga.

Huyu asisitiza kwamba shida kubwa ni usalama mdogo mashariki mwa DRC, yaani Kivu ya kaskazini na Ituri.

Akiongeza kuwa alikutanana na viongozi wa kijeshi na hata wana siasa ili kutafuta namna ya kukomesha kundi zenyi kumiliki silaha Kivu ya kaskazini na Ituri.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire