Kinshasa : Ujumbe wa Muungano wa ma askofu CENCO imekutana naye Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI

Kipande ya mji wa Kinshasa

Ujumbe wa Muungano wa ma askofu nchini DRC CENCO umekutana ijumaa tarehe 26 novemba na Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO.

Duru zetu toka mjini Kinshasa zanena kwamba mazungumzo yalihusu hali ya usalama na ya kisiasa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo.

Mbele ya wandishi habari Askofu Marcel UTEMBI anena ma askofu wanakusudia kutowa mwangaza vizuri kuhusu uongozi wa kijeshi katika majimbo ya Kivu ya kaskazini na ya Ituri.

Askofu Marcel UTEMBI aliyeongoza ujumbe asema kwamba ma askofu walitoa pendekezo kadhaa ili kuepuka mgomo katika sekta ya elimu. Na kuhusu uchaguzi, hawa walisisitiza harakati hiyo ifanyike, wakinena kuna wakati wa vita na wakati wa kujenga.

Duru zetu zafahamisha kwamba ujumbe huo uliundwa na askofu kumi na nane wa kikatoliki. Walishiriki pia kwenyi mazungumzo prezidenti wa bunge la taifa na ule wa seneti.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire