DRC- UGANDA: Operesheni za kukomesha wanamugambo wa ADF kwenyi DRC zimeanzishwa

Huku ni katika nchi ya Uganda

Nchi ya Uganda na DRC zimetangaza hii juma nne kuanzishwa kwa Operesheni ya pamoja kati ya DRC na nchi hiyo dhidi ya wanamugambo wa ADF mashariki mwa DRC.

Kutokana na nchi ya Uganda, hiyo ni mwanzo wa uhusiano kijeshi kati ya nchi hizo mbili.

Mnenaji wa jeshi la Uganda Bwana Flavien ahakikisha kwamba kutakuweko Operesheni zingine za kijeshi

Duru zingine toka Uganda hunena kwamba asubui mapema shambulizi la ndege lilijitokeza nchini humo hadi kwenyi kempi ya wanamugambo ADF wapatikanao mashariki mwa DRC.

Mji wa Kinshasa

Pamoja na hayo shambulizi la chini ili mara moja kukomesha swala la wanamugambo ADF kunako nchi ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Kuanzishwa kwa shambulizi dhidi wanamugambo ADF kwenyi udongo wa DRC ni matakwa ya nchi ya Uganda tangu awali.

Umoja wa kimataifa wahakikisha kuwa Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI alikubali jeshi la Uganda liweze kwendesha shambulizi dhidi ya wanamugambo ADF wapatikanao mashariki mwa DRC. Duru zetu zaongeza kwamba hiyo ni matokeo ya mazungumzo iliyoendeshwa hapa karibuni kati ya nchi hizo mbili.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire