Goma : Aubin MONGOLI aomba raia kuungana bega kwa bega ili ya kukomesha ukimwi

Mratibu wa shirika PNMLS kivu ya kaskazini Aubin MONGOLI

Tarehe mosi disemba kila mwaka, ulimwengu mzima washerekea siku kuu ya kupiganisha ukimwi. Mjini Goma, siku hiyo ilisherekewa kwenyi ofisi ya liwali wa Jimbo la kivu ya kaskazini.

Siku kuu ilisherekewa katika mada kimataifa :  » « Kukomesha hali ya ubaguzi na kujitahidi ili kukomesha ukimwi hapa mwaka 2030« .

Mratibu wa shirika la kupiganisha ukimwi PNMLS jimboni Kivu ya kaskazini Aubin MONGOLI afahamisha kuwa ni wagonjwa 181 ndio wamefariki dunia kutokana na ukimwi mwanzoni mwa mwaka 2021 kabla mwaka huo kukoma.

Huyu aomba raia kwa jumla kujihusisha katika kupiganisha maradhi hayo kwani watu wengi kwa sasa hufikiri tu kuhusu janga la Korona, Ebola na kadhalika wakisahau kwamba ukimwi inaendelea kuuwa.

Aubin MONGOLI agusia pia matatizo chungu tele ambayo shirika PNMLS lapitia kwa sasa. Akitaja ukosefu wa dawa hata kwa watoto, ubaguzi waishimo ndani wagonjwa wa ukimwi ndani ya jamii

Akiongeza kuwa Jimbo la kivu ya kaskazini laishi hali mbovu na hii ni moja wapo wa njia zenyi kurahisisha ukimwi jimboni humo.

Kiongozi wa PNMLS kivu ya kaskazini alinena kuhusu ukosefu wa wafadhili na hata mcango wa nyumbani ili kuendelea kukomesha ukimwi.

Akisisitiza kuhusu watu wanaofariki dunia pasipo kupata matibabu, wengine hujikuta ndani ya vyumba vya maombi , wengine kwa wafumu. N’a kwamba hayo yote ni udanganyifu mtupu.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire