Kivu ya kusini : Shauri ya chama Les républicains mashariki mwa DRC lanena kutounga mkono barua ya wanabunge kutaka kumuondowa madarakani liwali Théo Ngwabije na timu lake

Mratibu wa chama Les républicains pia mwandishi makamu wa chama hicho

Shauri ya chama cha kisiasa chake Léon Kengo wa dondo « Les républicains mashariki mwa DRC kupitia mratibu wake Mathieu Batumike Mpinike lilikutana juma mosi mjini Goma likitupilia mbali kibarua cha wanabunge. Kibarua kinachotaka aondoke madarakani liwali wa jimbo la kivu ya kusini Théo Ngwabije KASI na timu lake.

Shauri la chama hicho chake lasisitiza kuwa hiyo ni mizozo mtupu dhidi ya jimbo ili kuzuia maendeleo na kazi zake liwali Théo Ngwabije ambaye ajitahidi kuwasaka wahuni wenyi kukwamisha usalama jimboni mwake.

Habari kutoka mratibu wa chama Les républicains pia mwandishi makamu wa chama hicho, zaonyesha kwamba wakati jimbo la kivu ya kusini lashambuliwa na waasi, liwali na timu lake wakijiandaa kukomesha adui , wanabunge jimboni waanda mbinu kwa kukwamisha liwali na serkali yake kupitia kibarua.

Uratibu wa chama Les républicains jimboni Kivu ya kusini

Shauri hili kupitia mratibu wake Mathieu Batumike laomba vyama vya kisiasa na mashirika za kiraia kufanya iwezekanayo ili kibarua chenyewe kisipate nafasi maana kina hatarisha jimbo kupitia njama za watu wenyi nia mbaya.

Habari hizi zahakikisha kwamba ni kila miezi mitatu ndipo wanabunge jimboni Kivu ya kusini washambulia liwali Théo Ngwabije na timu lake kutaka aache madaraka.

Jambo hili laomba kila mwanainchi kukataa kata kata maana ni namna ya kuharibu maendeleo ya jimbo, zanena habari toka Shauri la chama Les républicains kupitia mratibu wake Mathieu Batumike MPINIKE pia mwandishi makamu wa chama hicho.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire