Akiwasili hii alhamisi tarehe 2 disemba mjini Goma, waziri ahusikae na ujenzi nchini DRC Alexis GISARO asema kuanzishwa kwa kazi za ujenzi wa barabara Kasindi Béni Butembo Bunagana Rutshuru Goma jimboni Kivu ya kaskazini.
Waziri afahamisha mbele ya wandishi habari kwamba wafanya kazi na vifaa tayari vimefikishwa mjini Goma ili ya kuanzisha rasmi kazi zenyewe.
Akihojiwa kuhusu usalama mdogo eneo hilo , huyu afahamisha kuwa wafanya kazi watalindwa na askari jeshi wa serkali FARDC. « Kazi hizo zalenga kuboresha maendeleo jimboni Kivu ya kaskazini » aongeza waziri.
Tukumbushe kwamba ni tangu mwezi juni iliyopita ndipo ma Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI na mwenziwe Yoweri Kaguta MUSEVENi walianzisha rasmi kazi za ujenzi wa barabara eneo hilo lenyi urefu wa kilomita 223.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.