Kivu ya kusini: Muungano wa wandishi habari jimboni UNPC walazimisha mapatano kuhusu wandishi habari walijeruhiwa mjini Bukavu

Tukiwa mbele ya ofisi ya bunge jimboni Kivu ya kusini.

Wapasha habari tatu walijeruhiwa kunako bunge jimboni Kivu ya kusini mbele ianzishwe mkutano wa heka heka uliopelekeya liwali wa Jimbo Théo Ngwabije na timu lake waondoshwe madarakani.

Katika kibarua chake , Muungano wa wandishi habari Kivu ya kusini UNPC unalaumu vitendo kama hivyo , kwa kuwa wapasha habari siyo wafanya siasa.

Muungano huo unaomba wandishi habari kufanya kazi yao vilivyo bila kujiingiza ndani ya siasa kwani siyo kazi yao.

Muungano wa wandishi habari UNPC unaomba viongozi wa jimbo wa sasa ama watakao kuja kujihusisha na swala la wandishi habari hao kuhusu haki yao.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire