Bukavu : Kongamano ya pili ya Muungano wa kisiasa nchini DRC BUREC itafanyika mjini humo

Prezidenti wa Muungano BUREC nchini DRC

Akiwasili mjini Goma toka mji mkuu Kinshasa, Prezident i wa Muungano wa kisiasa BUREC Jean Marie KASEREKA KATOKOLYO anena kufika mjini Goma, akielekea mjini Bukavu ambako Kongamano ya pili ya Muungano huo itafanyika tarehe 8 na 9 disemba 2021.

Mbele ya wandishi habari alifahamisha kwamba mji wa Bukavu ulichaguliwa kwa kuwa ni moja wapo wa miji ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Akiongeza kwamba katika siasa ya Muungano wa kisiasa BUREC ni kila miaka tano ndipo yafanyika Kongamano , na ni katika miji mbali mbali , na hii ni fursa kwa mji wa Bukavu.

Prezidenti wa BUREC nchini DRC alifahamisha kwamba Kongamano haiandaliwe kwa kuwa uchaguzi ni hapa karibuni, ingawa katika nchi ya kidemokrasia mfano wa DRC, vyama vya kisiasa hujiandaa ili kutekeleza mipango yao kupitia uchaguzi.

Fahamuni kwamba Kongamano hiyo ilibidi ifanyike mwaka 2020 ila kutokana na hali ya maradhi ya Korona haikufanyika.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire