Bukavu : Uratibu wa chama cha kisiasa Les républicains unasema kukerwa na hali ya kisiasa jimboni Kivu ya kusini

Kamati ya uratibu wa chama Les républicains Kivu ya kusini

Katika mkutano hii ijumaa tarehe 3 disemba 2021, Kamati ya uratibu wa chama cha kisiasa Les républicains jimboni Kivu ya kusini unasema kuhuzunishwa na hali ya kisiasa jimboni humo ambayo ni ya heka heka kati ya bunge la jimbo na serkali.

Kamati ya Uratibu kupitia mratibu mashariki mwa DRC ambaye pia katibu makamu wa chama Mathieu BATUMIKE MPINIKE na mwenziwe Dokta Romain Talkis waliosahini ujumbe, hunena kutohusika kwa mbali ama kwa karibu ama kutokubali matokeo ya uchaguzi uliofanyika kwenyi bunge, ambayo ni namna ya kukwamisha maendeleo Jimbo.

Kamati ya Uratibu wa chama Les républicains unanena kwamba bunge la jimbo liliweza kukiuka kipengele cha 62 mstari wa kwanza ya sheria ya bunge na sheria kuhusu uongozi huru wa jimbo.

Kamati ya Uratibu ya chama cha kisiasa Les républicains yaomba viongozi wa kisiasa na wale wa kisheria kujihusisha ili kutekeleza usalama jimboni Kivu ya kusini.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire