Goma : Julien PALUKU aomba kuunga mkono Jeshi la taifa FARDC

Waziri ahusikae na viwanda nchini DRC Julien PALUKU KAHONGYA

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma pili tarehe 5 disemba 2021, waziri ahusikae na viwanda nchini DRC Julien PALUKU KAHONGYA anena kuja mjini Goma ili kushiriki kwenyi Kongamano ya kisiasa inayoandaliwa mjini Bukavu.

Mkutano huo mkuu unaandaliwa na Muungano wa kisiasa BUREC tarehe 8 hadi tarehe 9 disemba ukijumwisha viongozi wengi wa chama hicho.

Katika matamshi yake mbele wandishi habari , waziri Julien PALUKU anena kuwa serkali ya DRC ina haja ya kujiunga na raia ili kupiga waasi wenyi kukwamisha usalama jimboni Kivu ya kaskazini na Ituri ili kutekeleza amani.

Ndipo aliomba raia kutumika bega kwa bega na Jeshi la taifa ili kufikia amani mashariki mwa DRC.

Tufahamishe kwamba waziri ahusikae na viwanda alipokelewa kwenyi uwanja wa ndege na shangwe na vigelegele na raia walio wengi.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire