Goma : Kijana moja huaga dunia kwa kufyatulia risasi

Mtaa wa Goma

Kijana moja mwenyi umri wa miaka zaidi ishirini afariki dunia baada ya kugongwa risasi na wanaozaniwa askari polisi pa kata Katoyi usiku wa juma pili kuamkia juma tatu tarehe 6 disemba 2021.

Duru za mahali zanena kwamba ilionekana hali ya vuta ni kuvute kati mhanga na hawa walinzi wa usalama. Wakitaka kumunyanganya simu yake ya mkononi kabla ya kutaka kuvamia mpenziwe.

Ndipo walimufyatuliya risasi na akafariki hapo hapo. Habari tunazo kwa sasa ni kwamba mwili wake walazwa kwenyi chumba cha wafu mjini Goma.

Tukumbushe jambo karibu na hili lilipitika huko Ngangi ya tatu si mbali na shule Kanaume wilayani Nyiragongo. Kijana mwenyi umri karibu 15 ajikuta kuzingirwa na askari polisi wengine ambao hawakufaulu kumunyanganya radio ndogo na kadi za kurikodi nyimbo ndipo kumuvuwa vazi wakisingizia kuwa ni la kijeshi.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire