Baada ya kuchaguliwa mara ingine sawa kiongozi wa Muungano wa kamati za wachuuzi jimboni Kivu ya kusini Étienne BUHENDWA anena kuwa atafanya yote iwezekanayo ili kuboresha kazi. Akiendelea kushukuru wote walio onyesha matumaini kwake wakimchagua kwa mhula mwengine wa miaka tatu.
Étienne BUHENDWA anena hayo kwa ripota wa la ronde info juma tano tarehe 8 disemba 2021 mjini Bukavu.
Akisema kuwa soko za jimbo zina matatizo chungu tele yaani wachuuzi wamoja kukataa kulipa ushuru kwa serkali, wengine hulipa ushuru kinyume na sheria, uchafu ndani soko zimoja na kadhalika
Prezidenti huyu wa Muungano wa kamati ya uongozi wa soko za jimbo atamka kuwa hakuna siri maalum katika uongozi ili kukubaliwa. Siri moja ni kuongoza kwa kujishusha ila siyo kujipandisha. Na kwamba mfano huu ni wa kuiga kwa viongozi wengine.
Pamoja na hayo Étienne BUHENDWA aahidi kufanya mzunguko kwenyi soko zingine jimboni siku za usoni, ili kuchukuwa malalamiko ya wachuuzi na kuyafikisha kwenyi ngazi za juu.
Na kuhusu shida kwenyi ya soko ya Nguba anayoiongoza binafsi, huyu aonyesha kuwa matatizo ni chungu tele. Mfano wa usafi ambao anaendelea kujihusisha, ujenzi wa nyumba za kuweka byashara za soko na kadhalika.
Étienne BUHENDWA aamini kwamba kiongozi wa mtaa wa Ibanda aliyeahidi ujenzi wa nyumba za soko hiyo atajihusisha bila Shaka. Tufahamishe kwamba atashimikwa rasmi tarehe 18 disemba 2021.
Juvénal Murhula
Qmmap0p
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.