Akihojiwa na wandishi habari hii juma tano tarehe 15 disemba 2021 kunako uwanja wa ndege pa Goma, waziri makamu husika na afya nchini DRC Bi Véronique KILUMBA anena kuja ili kushiriki kwenyi kikao kinacho lenga kupiganisha virusi vya ukimwi.
» Tumekuja kushiriki kwenyi kikao namna ya kusindikiza washiriki kwa kuandaa mbinu kwa kufikia lengo ifikapo mwaka 2030. Lengo ni kwamba raia waweze kufahamu hali yao kiafya, waweze pia kupata matunzo bora na kadhalika » anena waziri makamu wa afya.
Huyu aongeza kwamba pamoja, watafanya yote iwezekanayo ili kutekeleza maoni ya Raisi wa nchi Félix Antoine TSHISEKEDI.
« Sisi sote pamoja tutatekeleza matakwa yake Raisi wa nchi, kwa uongozi wa waziri mkuu. Washirika katika sekta ya afya, wizara ya afya tunayo ongoza, shirika la raia, mashirika mbali mbali sote tutajihusisha ili tufikie ukomo ifikapo mwaka 2030, » anena Bi Véronique KILUMBA.
Waziri makamu aongeza kwamba Raisi wa DRC na washirika kiufundi pamoja na wizara anayoiongoza wajitahidi ili hata raia wapatinao mbali vijijini wapate dawa dhidi ya maradhi ya ukimwi.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.