Goma: Guy KIBIRA arudi mjini humo akisindikizwa na viongozi wa vijana nchini DRC

Prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini Guy KIBIRA

Prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini Guy KIBIRA awasili hii alhamisi tarehe 16 disemba 2021 mjini Goma, toka mji mkuu Kinshasa. Akieleza mbele ya wandishi habari kwamba alikwenda huko ajili ya kutetea hali ya vijana jimboni Kivu ya kaskazini.

Huyu anena kwamba akuja na waziri husika na swala la vijana pamoja na prezidenti wa shauri la vijana nchini DRC, ambao watawasilli baadae.

Prezidenti wa shauri la vijana jimboni Kivu ya kaskazini asema kuwa alibaki Kinshasa akifanya utetezi kwenyi ngazi za sheria , kuhusu hasa kujipenya kwa kundi zenyi kumiliki silaha kwenyi eneo za DRC yaani Nyiragongo na Rutshuru.

« Tunarudi mjini Goma bila kufikia lengo maana Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI ametuma waziri husika na vijana pamoja prezidenti wa vijana nchini DRC kuja jionea binafsi jisi hali ya vijana ilivyo kwenyi majimbo ya kivu ya kaskazini na kusini, » anena kiongozi huyu

Pamoja na hayo waziri husika na swala la vijana atembelea senta kadhaa husika na mafunzo ya vijana jimboni Kivu ya kaskazini na kusini kwa kuwa ni moja wapo wa jukumu lake ili kupelekea vijana kujitegemea.

Prezidenti wa vijana Guy KIBIRA alaumu pia mauaji ambayo yaendelea fanyika mjini na jimboni ambayo yamepelekea maelfu ya watu kuuliwa. Akiomba viongozi wa tabaka za chini kuunga liwali mwanajeshi mkono, kwa kuwa yeye peke hawezi faulu. Kwa vijana kutumika bega kwa bega na viongozi wa usalama wakitoa habari mapema.

Guy KIBIRA afahamisha mwishowe kwamba ni mhimu kuweko kwa ma askari wa Rwanda na Uganda nchini DRC kwa kusaidia Jeshi la Kongo ingawa wataweza kutekeleza amani mashariki mwa nchi. Na kama sivyo vijana watatoa kauli.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire