Goma : Mwanabunge Hubert FURUGUTA atoa maoni kuhusu hali ya kisiasa nchini DRC

Mwanabunge Hubert Furuguta mchaguliwa wa Goma

Mwanabunge Hubert FURUGUTA anena kuwa sheria ya DRC imefanya kazi yake kwa kumuachilia huru kwa muda Prezidenti wa chama UNC Vital KAMERHE. Huyu angojea kuachiliwa rasmi kwake maana ana kazi kubwa nchini mwake.

Mchaguliwa wa Goma Hubert Furuguta atamka hayo hii alhamisi tarehe 16 disemba 2021 kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma toka mji mkuu Kinshasa.

Akihojiwa kuhusu usalama mdogo unaotanda kiasi mjini Goma, mwanabunge asema kwamba ndiyo sababu ya kuja kwake mjini ili kupongeza jamaa hizi na raia wote kuhusu hali ya mauaji.

« Ninaamini uongozi wa zarura unafanya nguvu ili mambo yabadili. Mara tunatoka poteza ndugu zetu , hali hii haipashwi iendelee. Tunaomba sheria ya kijeshi hata na viongozi wanajeshi kujihusisha zaidi ili kugunduwa wahusika na mauaji, ili mabadiliko kamili « anena Hubert Furuguta mchaguliwa wa Goma.

Kuhusu wabunge wa taifa wamoja wanaopinga kuweko kwa askari wa Rwanda na Uganda nchini ili kusaidia jeshi la taifa, mwanabunge huyu anena kuwa raia wana hitaji amani.

« Raisi wa DRC aliahidi amani ambayo anaendelea kusaka. Jambo hili halifurahishe watu wamoja. Miaka thelasini na saba ya upinzani inabidi Raisi kutekeleza amani nchini . Ingawa hakuna suluhu , tutachukuwa kauli Anena Hubert Furuguta.

Mwanabunge huyu azani kwamba inabidi wana elimu kutupilia mbali tabia ya kuteta bali kutoa maoni ambayo itasaidia Raisi wa nchi kuleta mabadiliko ya kudumu.

‘Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire