Goma: Waziri husika na maswala za vijana nchini DRC yupo ziarani jimboni Kivu ya kaskazini na kusini

Waziri husika na swala za vijana nchini DRC Yves Bunkulu

Akiwasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii ijumaa tarehe 17 disemba 2021, waziri husika na maswala za vijana nchini DRC Yves BUNKULU ZOLA anena mbele ya wandishi habari ,kuja jimboni Kivu ya kaskazini na kusini ili kujionea binafsi hali waishimo vijana maeneo hiyo.

Kuhusu mauaji za vijana kila leo mjini Goma na ndani ya jimbo, waziri atoa mbele ya yote ujumbe wa rambi rambi kwa jamaa zilizokumbwa na msiba.

Yves BUNKULU aomba vijana kutumika bega kwa bega na askari wa mahali ili kukomesha usalama mdogo ndani ya majimbo ya kivu ya kaskazini na Ituri zilizo katika uongozi wa zarura.

« Vijana waombwa kutoa hazarani adui anayejificha miongoni mwao ili amani irudi bila shaka ndani ya jimbo letu » aongeza waziri.

Kuhusu kundi za vijana ambazo hazina viongozi kwa sasa, waziri husika na maswala za vijana Yves BUNKULU atamka kuwa swala aina hiyo itagusiwa kwa kuwa ni moja wapo wa lengo kufika jimboni Kivu ya kaskazini na kusini.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire