Goma : Emmanuel Gashamba anena kufurahishwa na matokeo ya mtihani elimu ya kiufundi Kivu ya kaskazini ya kwanza

Inspekta mkuu husika na mafunzo ya kiufundi Kivu ya kaskazini ya kwanza Emmanuel Gashamba

Inspekta mkuu husika na elimu ya kiufundi Kivu ya kaskazini ya kwanza Emmanuel Gashamba asema kuwa na furaha kubwa baada ya kushiriki mjini Kinshasa kwenyi sherehe ya kutangaza matokeo ya mtihani kipindi cha kwanza kwa mafunzo ya kiufundi nchini DRC. Baada ya miezi mitatu tangu ifanyike mtihani huo. Na hii ni moja wapuo katika Historia ya Kongo.

Alinena hayo hii juma tano tarehe 22 disemba mjini Goma mbele ya wandishi habari, siku moja baada ya kutoka mjini Kinshasa.

« Tunasema aksanti kwa aliko toka waziri husika na elimu ya kiufundi nchini DRC. Aliomba tufike mjini Kinshasa kwa kusindiza wanafunzi 15 waliofaulu kwa asilimia themanini hadi tisini. Tunapiga pia aksanti kwake waziri mkuu aliyewakilisha sherehe, kwa kumheshimisha waziri husika na mafunzo ya kiufundi na hata wanafunzi waliofalau na wale hawakufaulu. Walio faulu zaidi walipewa vifaa vya kazi kutokana na elimu waliofunzwa, pesa za shule, na kadhalika » , Anena Inspekta mkuu Emmanuel Gashamba.

Kwake , waliopinga mafunzo ya kiufundi, kwa kweli wamejioneya wenyewe, kwa kuwa kazi itaendelea kusonga mbele miaka ijayo.

Akisisitiza kwamba ni jambo la kipeke kwani miongoni mwa akina mama 112 walioshiriki mtihani Kivu ya kaskazini ya kwanza, 97 wamejinyakulia ushindi.

Kiongozi huyu husika na mafunzo ya kiufundi Kivu ya kaskazini ya kwanza atoa mwito kwa wakandideti kuja kuchukuwa matokeo ya kazi zao wakilipa elfu 6 franka za Kongo.

« Pesa hizo zitapelekwa mjini Kinshasa kwa kuwa widhara husika na elimu ya kiufundi imesahini makubaliano na shirika moja la mawasiliano AFRICEL ambalo halipatikane kote nchini DRC », asema Emmanuel Gashamba. Tufahamishe kwamba ofisi ya uchunguzi kuhusu elimu ya kiufundi Kivu ya kaskazini ya kwanza yapatikana kwenyi mtaa wa Karisimbi mjini Goma.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire