Goma: Celestin Mvunabandi atoa hongera kwa raia wa Jimbo la Kivu ya kaskazini hususan kwa wale wa Rutshuru wanaokumbwa na usalama mdogo

Mwana seneti Célestin Mvunabandi kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma

Akija Goma hii ijumaa tarehe 24 disemba toka mji mkuu Kinshasa, mwana seneti Célestin Mvunabandi Prezidenti wa chama cha kisiasa ACN nchini DRC , anena kuwa likizoni mjini Goma kushiriki sherehe za mwisho wa mwaka pamoja memba wa chama na hata raia akitowa pole kwao kuhusu usalama mdogo unaowakumba.

Ilikuwa kwenyi uwanja wa ndege wa Goma mji mkuu wa Jimbo la kivu ya kaskazini.

« Nimekuja hapa nikiwa likizoni na kusherekea mwisho wa mwaka pamoja na wachaguzi wangu » anena mwana seneti Célestin Mvunabandi.

Kuhusu raia wenyi kusumbuka kila leo na usalama mdogo wilayani Rutshuru eneo lake , Célestin Mvunabandi atoa mbele ya yote pole kwa raia wa huko kutokana na shida hiyo.

Mwana seneti huyu aongeza kuwa serkali ya DRC yajitahidi kutafuta suluhu kuhusu usalama mdogo unaoripotiwa kila leo wilayani Rutshuru. Akiomba raia wa huko kuwa na matumaini na kusubiri hasa.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire