Robert Seninga amesisitiza kuhusu usalama mdogo jimboni Kivu ya kaskazini alipo shiriki kwenyi Kongamano ya ma liwali

Prezidenti wa bunge la Kivu ya kaskazini Robert Seninga anena kwamba amefikisha malalamiko ya raia wa jimbo lake kuhusu usalama mdogo unaowakumba. Ni wakati wa Kongamano ya ma liwali mjini Kinshasa iliyo ongozwa naye Raisi Félix Antoine TSHISEKEDI.

Prezidenti wa bunge anena hayo alipowasili kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma kutoka mji mkuu Kinshasa.

« Unajua usalama ni jambo linahusu hasa serkali ya taifa. Kwa hiyo tuliomba viongozi wa serkali kufanya yote iwezekanayo ili kutekeleza amani mashariki mwa DRC hususan katika majimbo ya Kivu ya kaskazini, kusini na Ituri « . Aeleza Kiongozi huyo

Akihojiwa kuhusu kusimamishwa kwa vibarua vinavyoondowa maliwali kazini na hata vile vinaomba kujifasiria bungeni , Prezidenti wa bunge anena kuwa ni jambo lisilo wezekana maana ni namna yake Raisi kukiuka sheria ya nchi.

Robert Seninga aongeza kwamba Raisi wa DRC aliomba maliwali uongozi bora, kutumia vizuri mali ya serkali ili kufikia maendeleo ya kweli. Na kwamba kikao kililenga ustawi wa majimbo za DRC na kupelekea maendeleo ya kudumu.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire