Goma: Promesse Matofali anena kuwa chama cha kisiasa Ensemble pour la République tayari kwenyi uchaguzi mwaka 2023 ili kubadili hali mbovu waishimo wakongomani

Mwanabunge Promesse Matofalli kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma

Mwanabunge jimboni Kivu ya kaskazini Promesse Matofali anena kwamba hali ya chama cha kisiasa Ensemble pour la République ni bora zaidi. Na kwamba kinajitahidi kunako uchaguzi wa mwaka 2023 ujao.

Mchaguliwa huyu anena hayo hii juma pili tarehe 26 disemba akitokea jimboni Tshopo na kandokando ambako wanamemba yaani ma kada wa chama hicho walialikwa naye Prezidenti wao Moïse Katumbi TCHAPWE.

Tunatoka mjini Kisangani ambako tuliitwa na Prezidenti wa chama chetu Ensemble pour le changement Moïse Katumbi ili ya kupanga kazi pamoja kwa kuwa muda umetimu anena Promesse Matofali.

Akiongeza kwamba hali ya chama ni nzuri na inabidi kitande kwenyi eneo mbali mbali za Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kuwa tayari kwa uchaguzi mwaka 2023 ujao.

Akihojiwa kuhusu usalama mdogo ambao ni shida chungu tele jimboni Kivu ya kaskazini na penginepo , mwanabuge huyu alionekana kusikitika maana Jeshi la Kongo lafanana kushindwa kila leo mbele ya adui. Jambo ambalo serkali ingebidi kuchunguza kwa makini ili raia waishio mashariki mwa DRC wapate amani ya kudumu.

Tufahamishe kwamba chama Ensemble pour le changement kwa kimombo chake Moïse Katumbi kinakuwa na mizizi yake karibu kwenyi eneo lote la Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire