Bukavu : Shirika nyipya la raia NDSCI lalaumu kusimamishwa kwa kazi za ulalo Mugaba

Mtaa wa Bagira

Shirika nyipya la raia NDSCI lapiga debe kuhusu kusimamishwa kwa kazi za ujenzi wa ulalo Mugaba ambao unaunganisha Kasha na mtaa wa Bagira na hata eneo zingine mjini Bukavu na jimboni Kivu ya kusini.

Kazi za ujenzi wa ulalo huo zilisapotiwa na serkali ya jimbo la Kivu ya kusini kwa utawala wake Théo Ngwabidje Kasi.

Kutokana na shirika nyipya la raia la kupitia mnenaji makamu wake jimboni Kivu ya kusini Wilfried Habamungu, vibambazi vya ulalo tayari vimesimama ila nafasi ya chini yabaki.

Ndio maana Shirika hili la kutetea haki ya binaadam laomba waziri husika na mambo ya ndani Kivu ya kusini pamoja na liwali makamu kufanya yote iwezekanayo ili kuhitimisha kazi za ujenzi.

Shirika nyipya la raia lasisitiza kwamba ulalo huo ni wa samani kubwa kwa kurahisisha mawasiliano kati ya wilaya kadhaa za jimbo na mji wa Bukavu kwa jumla.

Kufwatana na Wilfried Habamungu, raia wa eneo hilo wangojea kutolewa rasmi ulalo, kwa kuwa liwali wa jimbo Théo Ngwabidje Kasi aliahidi kwa wakaazi siku makumi sita ili waanze tumia ulalo wenyewe.

Kwa hiyo NDSCI aomba viongozi wa jimbo kufanya yote iwezekanayo ili vifaa vya kazi vilivyo baki chini visije vikapelekwe na wevi.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire