Goma: Mwanabunge Ayobangira Safari apatikana likizoni jimboni Kivu ya kaskazini ili kusherekea mwisho wa mwaka

Mwanabunge wa taifa Ayobangira Safari yuko likizoni mjini Goma ili kusherekea mwisho wa mwaka na wachaguzi wake Aliweza kujibu kwa maswala kadhaa ya wandishi habari kwenyi uwanja wa ndege mjini Goma hii juma nne tarehe 28 disemba 2021.

Kuhusu hali ya usalama jimboni Kivu ya kaskazini, Mwanabunge aonyesha kuwa ni yenyi kuzorota. Akiwa na matumaini kuhusu nguvu za pamoja kati ya jeshi la DRC na lile la Uganda ambazo zaendelea kugonga wanamugambo ADF. Na kwamba matumaini yako siku za usoni, ili kazi zifanyike kwa amani.

Kuhusu milioni elfu kumi dola za marekani kwa wilaya iliyozungumzwa ndani ya kongamano la maliwali mjini Kinshasa, Mwanabunge huyu anena kuwa ni vema ijapo wengi huzani kwamba DRC ni Kinshasa peke.

« Watu wengi huzani kwamba Kinshasa peke ni DRC nzima. Ingawa kila wilaya itapata dola milioni kumi za marekani , ni vema kuhusu maendeleo ya nchi. Mara kwa mara viongozi husahau eneo zimoja miaka na miaka jambo ambalo hukwamisha maendeleo » anena mchaguliwa wilayani Masisi.

Akihojiwa kuhusu matokeo ya ripoti ya likizo aliyoifanya mbeleni, Ayobangira Safari anena kuwa jambo hilo halikugusiwa kutokana na hali ya uongozi wa zarura jimboni, ila litaweza kutekelezwa badae.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire