Bukavu : Shirika nyipya la raia chumvi ya Kongo NDSCI lapanza sauti kuhusu hali mbovu kisiasa jimboni Kivu ya kusini

Katika tangazo lake la tarehe 30 disemba 2021, Shirika nyipya la raia NDSCI lanena kufwatilia kwa makini hali kasiasa yenyi kuzorota kiasi jimboni Kivu ya kusini. Hayo kutokana na migogoro kati ya serkali na bunge jimboni humo.

Tangazo hilo lenyi kusahiniwa na kamati ya uongozi wa NDSCI jimboni Kivu ya kusini, laangazia kuwa tangu bunge la jimbo litowe barua ya kuondowa madarakani serkali yake liwali Théo Ngwabidje hali tayari imekwama zaidi.

Upande mwengine serkali ya jimbo ikiegemea upande wa korti kuu ya jimbo iliyochukuwa hatua ya kurudisha serkali hiyo madarakani, wakati bunge lapinga katakata hatua hiyo. Pamoja na hayo mizozo kati ya viongozi wa mahali, wakitupiana matusi mitandaoni, matusi pia wafwasi kwa wafwasi wao.

NDSCI aomba Raisi wa DRC kujihusisha na hali mbovu inayokumba Jimbo la kivu ya kusini, kutofautisha serkali na bunge kulingana na sheria.

Kwa vijana kujitenga na wafanya siasa ambao wapigania faida zao binafsi wakiwa madarakani.

Kwa wahusika na migogoro kuweka silaha chini maana jimbo haliweza kuinuka katika mizozo. Kukaa hasa kwenyi meza wakiambia ukweli kwa manufaa ya raia.

Mwishowe Shirika nyipya la raia laomba wahusika kuvumiliana, kila mtu akitowa kauli, na kama sivyo jimbo halitajengwa.

Chumba cha uhariri

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire