Goma: Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo itainuka kiuchumi viongozi wakimupenda Mungu na wakimupenda jirani. Mtumishi wa Mungu Prince HANGI AMINI)

Mtumishi wa Mungu Prince HANGI AMINI anena kuwa inabidi viongozi wa nchi waende kwenyi baba zao wa imani ili wapewe shauri ila siyo baba wa imani kuwaendea viongozi ambao ni watoto wao wa imani. Hii itapelekea nchi kuinuka na raia wataishi maisha bora.

Mtumishi wa Mungu Prince HANGI AMINI anena hayo kwa ripota wa la ronde info juma hili, kulingana na hali mbovu ya maisha ya raia wa DRC miaka chungu tele.

Akihojiwa kuhusu maisha mabaya ya wakongomani ijapo wengi miongoni mwa viongozi wa nchi ni wakristu wa kanisa mbali mbali, mtumishi wa Mungu anena kuwa kanisa zaonekana katofanya kazi zao vilivyo. Watumishi wa Mungu wengi wengi waonekana chini ya mamlaka ya viongozi wa nchi ambao ni watoto wao wa imani, wakitafuta faida zao.

Kwake Prince HANGI AMINI, inabidi baba wa imani wachukuwe jukumu lao, kuendelea kuwafunza viongozi kupenda nchi yao.

Huyu aligusia neno la Mungu katika kitabu cha Matayo 22, 37-39; umupende Mungu na umupende jirani yako. Akisisitiza kwamba kwamba kumupenda jirani ni kupenda nchi, wakati unamupenda jirani hauwezi kumutakia maisha mabaya. Kwamba utatenda mema ajili yake.

Kwa mtumishi wa Mungu kuongoza nchi, Prince HANGI AMINI aeleza kwamba haiwezekane mtumishi wa Mungu akatumikie ma Bwana wawili maana atashindwa. Ingawa ameitwa na Mungu kufanya hudumu sherti abaki kwenyi msimamo huo, na kama atafanya siasa ya nchi abaki kwa kazi hiyo.

Prince HANGI wa kanisa Salut par la Foi en Jésus Christ aeleza kuwa inabidi vijana wafunzwe siasa na waangaziwe na neno la Mungu ili watumikie vema nchi. Na wale walioitwa kwa huduma ya kanisa waifanye pasipo kuchanga na siasa.

Kwa mwisho, mtumishi wa Mungu Prince HANGI AMINI aomba raia kuwachaguwa viongozi wenyi kupenda na kutumikia nchi. Kwa wafanya siasa kupenda nchi na kutumika kwa manufaa ya raia siyo kwa manufaa yao binafsi. Na kwa viongozi wa kanisa kuchukuwa jukumu lao, wakiwaonya viongozi wa nchi ambao ni watoto wao wa imani, si wao kujishusha ili hali isiendelee kuzorota kiasi

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire