Goma : Viongozi wa DRC wamupende Mungu na wapende nchi yao ili kuboresha hali ya maisha ya raia

Mtumishi wa Mungu Prince HANGI AMINI wa kanisa Salut par la Foi en Jésus Christ

Inabidi viongozi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwenda kuomba shauri kwa watumishi wa Mungu ambao ni baba wa imani. Siyo watumishi wa Mungu kwenda kwenyi viongozi wa nchi ambao ni watoto wao wa imani. Hayo yatapelekea uongozi bora wa nchi na itakuwa furaha kubwa kwa raia.

Ni matamshi yake mtumishi wa Mungu Prince HANGI AMINI akihojiwa na ripota wa la ronde info hii juma mosi tarehe mosi januari 2022 mjini Goma.

Mtumishi wa Mungu anena kuwa kanisa hazifanye kazi ipasavyo, ndio maana DRC yaendelea kukumbwa na shida chungu tele.

« Watumishi wengi waonekana kuwa chini ya mamlaka ya viongozi wa nchi kwa faida zao binafsi , na hayo huharibu nchi nzima  » anena Prince HANGI AMINI.

Pamoja na hayo, aonyesha kwamba inabidi vijana wamoja watakao ongoza nchi wafunzwe siasa, pia watumike wakimuogopa Mungu. Akiongeza kwamba walioitwa kwa huduma za kanisa wazifanye pasipo kuchanga siasa.

Prince HANGI AMINI mtumishi wa kanisa Salut pour la Foi en Jésus Christ agusia neno la Mungu kitabu cha Matayo 22, 37-39 ikituamuru kumupenda Mungu na kumupenda jirani.

Prince HANGI aendelea sisitiza kuhusu upendo wa nchi. Kwa raia aomba kuchagua viongozi wanaofaa, wenyi kuogopa Mungu, wanaopenda nchi. Kwa viongozi wa nchi, kuogopa Mungu wakitumika kwa manufaa ya raia. Kwa watumishi wa Mungu, kuchukuwa jukumu lao, wakionya viongozi wa nchi ambao ni wakristu wao, wasiweze kujishusha mbele yao.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire