Bukavu : Shirika nyipya la raia NDSCI lapinga vizuizi vya askari jeshi mjini Bukavu na jimboni Kivu ya kusini

Wilfried Habamungu mnenaji makamu wa shirika nyipya la raia NDSCI Kivu ya kusini

Shirika nyipya la raia kupitia mnenaji wake makamu Wilfried Habamungu lapinga kuweko kwa vizuizi pa Rugondo katika kata Mulwa mtaani Bagira. Pia kizuizi kwenyi barabara Nafasi ya uhuru hadi Kavumu mahali iitwayo Kazingo.

Shirika hili laangazia kwamba mwezi disemba 2021 , askari Jeshi wameweka kizuizi pa Rugondo, wakilazimisha kwa kila mpita njia 500 ama 1000 franka za kongo. Na kuongeza kwamba hata wachuuzi toka Kabare wenyi kupeleka byashara yaani miwa, makaa, miti, mboga za majani na kadhalika walazimisha kuacha nusu ya byashara ama pesa.

NDSCI asema kuwa watu hawa ni wenyi huzuni kubwa maana walipa ushuru sokoni baadae kusumbulia na askari jeshi.

Shirika NDSCI laongeza kwamba hali kama hii yaonekana kwenyi barabara Nafasi ya uhuru hadi Kavumu eneo la Kazingo.

Duru toka eneo hilo zatamka kwamba askari jeshi walazimisha kwa madreva na waendesha pikipiki franka za kongo 500 hadi 2000. Hawa waacha kucunguza ndani ya gari kama vile walikuwa wakitumika mwanzoni mwa musako.

Shirika NDSCI kupitia Wilfried Habamungu laomba viongozi wa kijeshi yaani Jenerali wa eneo la thelasini na tatu la kijeshi kukataza tabia hiyo ambayo ni usalama mdogo kwa raia.

Kwa liwali makamu pamoja na waziri husika na usalama jimboni, kufanya yote iwezekanayo ili kulinda usalama wa raia. Mwishowe NDSCI aomba raia kutowa kila yeyote yule mwenyi kutaka kuvuruga amani jimboni wakishirikiana na vyombo vya usalama.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire