DRC : Christophe Lutundula aweka mkazo kwa diplomasia ili ya kutafuta suluhu kuhusu wakongomani wanaotupwa nje nchini Angola

Ni tangu wiki kadhaa wakongomani waishio nchini Angola wameanza kutupwa nje, ila serkali ya DRC hunena kuchagua njia ya kideplomasia ili kuleta suluhu pahali pa kujilipishia kisasi.

Ndivyo afahamisha kwa wenzetu wa Top Congo waziri husika na mambo ya nje mjini Kinshasa Christophe LUTUNDULA.

Kiongozi huyu husika na swala za kidiplomasia aonyesha kuwa serkali yajihusisha kutafuta suluhu ya pamoja na Angola.

Waziri anena kwamba inabidi serkali ipate habari kamili kuhusu swala hilo na kwamba wanaendelea kuwasiliana na viongozi wa Angola. Huyu aongeza kuwa ni tangu miaka kadhaa wakongomani wafukuzwa nchini humo, ingawa kutafuta suluhu kideplomasia.

Waziri husika na mambo ya nje asema kuwa kwenda uhamishoni ni kawaida na hii ni kutokana na shida ya maisha kwa wakongomani.

 » Kwenda uhamishoni hailete suluhu la kudumu kwa wanainchi. Wakongomani wapaswa baki makwao wakihitaji uongozi bora na kazi. Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI pamoja na serkali yake waziri mkuu Sama Lukonde wajitahidi kupata suluhu kuhusu shida île « anena waziri.

Kulingana na shida ya wakongomani huko Angola, waziri ameomba wenzake nchini humo kutatua swala hilo kideplomasia , yote yaweze fanyika katika uhusiano bora. Akiendelea kuweka mkazo katika kuboresha hali ya maisha nchini DRC.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire