Kivu ya kusini: Mkutano wa kujifahamisha kati ya viongozi wapya wa shule za msinji sekondari pia kiufundi EPST pamoja ya kamati ya sekta hiyo

Viongozi wapya wa shule za msinji, sekondari pia kiufundi EPST jimboni Kivu ya kusini wamekutana majuzi na kamati ya sekta jimboni humo ajili ya kujifahamisha wenyewe kwa wenyewe.

Bwana Roger MATABARO katibu wa kutetea haki ya walimu jimboni Kivu ya kusini SYECO kwa kimombo afahamisha kwamba viongozi wapya ni yule husika na shule za msinji, sekondari pia kiufundi, yule husika na mishahara ya walimu kwa kimombo SECOPE pamoja na Inspekta mkuu jimboni.

Roger MATABARO anena kuwa yote yalianza kwa kujifahamisha moja kwa moja katika mkutano.

Akiongeza kwamba baada ya hapo, kiongozi husika na idara ya elimu ya msinji, sekondari pia kiufundi alionyesha mradi wa kalenda inayosahiniwa na ambayo kazi zitakomeshwa na kamati inayotajwa kwa kutumika.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire