Akipatikana ziarani mjini Goma, wziri anayehusika na kilimo, uvuvi na ufugo Adrien BOKELE anena kuja humu jimboni ili kuchunguza hali ya kazi.
« Nakuja humu jimboni Kivu ya kaskazini ili kuchunguza hali ya kazi. Ya pili ni swala la wavuvi wakongomani wanaotatizwa toka nchi ya Uganda. Wakati tunapatikana mjini Kinshasa kila mara ripoti zaeleza kuhusu kufungwa kwa wavuvi wakongomani na nchi ya Uganda kunako ziwa Édouard. Sasa nakuja kujionea binafsi jisi hali ilivyo . Punde si punde nitakutanana na waziri husika na uvuvi jimboni pamoja vyombo vya usalama ili kutafuta suluhu kuhusu shida za wavuvi. » Aeleza Waziri.
Akihojiwa kuhusu siasa yake ili kutekeleza amani ndani ya sekta hiyo kwani wavuvi watatizwa kila leo, waziri ahakikisha kwamba siasa anayo.
» Siasa tunayo. Shida ni mpaka kati ya DRC na nchi ya Uganda. Sisi tutakaa kwenyi meza na viongozi wa Uganda. Tunaamini kwamba suluhu litapatikana kwa kuwa hata wafadhili wetu wapatikana huko « aeleza waziri Adrien BOKELE.
Juvénal Murhula
»
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.