DRC : Joseph Kabila raisi wa zamani wa Kongo atakuwa mbele ya korti kuu ama la mjini Kinshasa

Habari toka mjini Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo zaendelea kunena kwamba korti kuu ya kijeshi itaamuwa hii juma tano tarehe 19 januari 2022 kuhusu kusambishwa ama la kwake Raisi wa zamani Joseph Kabila Kabange.

Raisi wa zamani Joseph Kabila Kabange wa DRC

Huyu akishutumiwa kusababisha mauaji yake mtetezi wa haki ya binaasam Flobert Chebeya pamoja naye Fidèle Bazana.

Katika kesi hiyo moja wa washuhuda alimtaja Raisi wa zamani Joseph Kabila Kabange kujihusisha na mauaji hayo.

Wadadisi wa mambo tulio wahoji hapa na pale wanena kwamba ingawa Raisi atawekwa mbele ya vyombo vya sheria na kufanya uamzi ulio halali, itakuwa mfano kwa viongozi wengine wa DRC ambao huzani kuwa juu ya sheria ajili ya pesa.

Wengine husema kuwa wanangojea wakatazama maana sheria ya Kongo huegemea mara kwa mara upande wa wenyi nguvu yaani matajiri na viongozi wa tabaka za juu.

Wanasema kusubiri mwanzo hadi mwisho ambayo ni uamzi kwa jumla katika kesi hiyo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire