Goma: Raia wakumbuka wak kiongozi wa kata Mabanga ya kusini mwaka moja baada ya kufariki kwake

Patrick Mundeke mshauri husika na swala za vijana upande wa Moïse Katumbi

Wanabunge kadhaa wa taifa na jimboni Kivu ya kaskazini wamandaa sherehe ya kumbukumbu mwaka moja baada ya kuaga dunia kwake Joseph Ikando aliyekuwa kiongozi shujaa wa kata Mabanga ya kusini mjini Goma.

Misaada kadhaa tayari zimetolewa kwa jamaa la ayati Joseph Ikando , tukitaja nyumba, pesa, vifaa vya kujenga kaburi, kusapoti kijana wa kwanza wa marehemu kwenyi univasti na kadhalika.

Sherehe ilifanyika hii juma tano tarehe 26 januari mjini Goma baada ya kutembelea kwenyi shamba la wafu ambako ulizikwa mwili wa marehemu.

Patrick Mundeke mshauri husika na swala la vijana upande wa Moïse Katumbi ambaye ni moja wa vijana wa kata Mabanga ya kusini aahidi mifuko thelasini ya saruji yaani ciment mcango ajili ya ujenzi wa kaburi yake ayati Joseph Ikando kwa kongojea. Akishukuru wale wote walionyosha mkono ajili ya jamaa iliyoachwa.

Kwake Patrick Mundeke : » Ayati Joseph Ikando aliye kiongozi wa kata Mabanga ya kusini hakukuwa na bajeti fulani, hata mshahara ila aliweka matumaini kwa raia walio wengi. Ijapo wanao mali watowa ahadi siku kwa siku pasipo kutenda lolote lile . Nashakuru shauri la vijana mjini Goma kwa kuandaa sherehe hii « asisitisa Patrick Mundeke.

Jamaa ya ayati Joseph Ikando aliye kiongozi shujaa wa kata Mabanga ya kusini

Jamaa la ayati Joseph pamoja na shauri la vijana la mahali walishukuru kwa huduma ya wabunge hawa na watu wengine wa moyo mwema ajili ya jamaa.

Tufahamishe kwamba kazi micezo ya kandanda, kazi za usalama , maendeleo na huduma kwa jamaa zinaandaliwa ajili ya kumbukumbu hiyo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire