Béni: Mauaji ya raia zaidi ishirini yaripotiwa mara ingine

Pande moja ya mji wa Beni

Watu wenyi kumiliki silaha wakizaniwa wanamugambo ADF wamewauwa raia zaidi ishirini katika vijiji vya Kandiasa, Kakutama na Ngobu kwenyi umbali wa kilomita tano toka Mantumbi tukiwa ndani ya sekta Mbau Béni.

Duru toka hapa na pale zaangazia kwamba wahanga walikutwa shambani wakifanya kazi yao. Ijapo wengine wengi haijulikane mahali walipo, wakizaniwa kupelekwa msituni.

Akizungumza kwenyi vyombo vya habari, Kavua Yalala husika na maendeleo vijijini anena kuwa Jeshi la taifa liliwahi gunduwa nafasi walipofichama magaidi hawo, Ndipo mituto ya silaha kati ya pande hizo mbili ilianza.

Duru hiyo husema kutofahamu matokeo ya mapigano kati ya pande hizo mbili husika.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire