Goma : Mwanabunge Josué Mufula ameachiliwa huru kwa muda

Mwanabunge Josué Mufula mchaguliwa wa Goma

Habari tunazo kwa sasa ni kwamba mwanabunge Josué Mufula mchaguliwa wa mji wa Goma ameachiliwa huru kwa muda na mahakama ya kijeshi ya Jimbo la Kivu ya kaskazini.

Akishutumiwa ucokozi. kutoheshimu viongozi wa serkali na matusi dhidi ya askari jeshi wa taifa huyu ameachiliwa huru. Korti ya kijeshi kujiswali bila mamlaka katika uamzi wa mubunge wa taifa.

Jambo ambalo watetezi wake waliangazia vyombo vya sheria tangu jana tarehe 8 februari 2022. Wakisisitiza kuwa hii ni ukiukaji wa katiba kipengele cha 19. Kinachoomba mshutumiwa aweze kusamba mbele ya muamzi wake husika pahali pa muamzi wa tabaka za chini.

Tufahamishe kwamba Josué Mufula alizuwiliwa jana na mashirika ya usalama, kupanda ndege hadi mjini Kinshasa ajili ya kazi.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire