
Josué MUFULA mwanabunge wa taifa akisikilizwa tangu hii juma tano tarehe 8 februari 2022 na mashirika ya usalama mjini Goma jimboni Kivu ya kaskazini.
Huyu alizuwiliwa kupanda ndege kwenyi uwanja wa Goma na mashirika ya usalama alipotaka kujielekeza mjini Kinshasa .
Duru za hapa na pale hunena kwamba mwanabunge huyu wa taifa ashutumiwa uchokozi, kutoheshimu viongozi wa serkali na matusi dhidi ya Jeshi FARDC.
Duru za karibu naye Josué MUFULA hunena kwamba huyu amefunguliwa kesi kutokana na kujingiza ndani ya swala lililolazimisha madreva wa mji kupakaa kila gari rangi ya kimanjano. Jambo lililozorotesha sekta ya uchukuzi mjini Goma siku kadhaa.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.