Ituri: Ngome za ADF zashambuliwa na Jeshi la Uganda kwa mituto ya risasi

Mji wa Bunia

Ngome za Uganda katika pori la Makolomakolo upande wa Zunguluku katika mji wa Irumu liliweza shambuliwa na Jeshi la Uganda.

Duru toka eneo hilo zaangazia kwamba milio ya silaha kubwa kubwa ilisikika pande nyingi kusini mwa Irumu na kutia hofu ndani ya wakaazi.

Duru za Jeshi la taifa FARDC zahakikisha kuwa mpango wa operesheni za pamoja FARDC na PDF tayari umeanzishwa ili kuteketeza maadui ADF eneo hilo.

Msemaji wa FARDC pa Ituri aomba raia kubaki kimya kwani operesheni hizo zina lengo la kutekeleza amani maeneo hayo.

Kwa ukumbusho ni tangu tarehe 20 januari 2022 ndipo Jeshi la PDF la Uganda lilivuka mto Semliki na kuingia jimboni Ituri katika lengo la kuweka nguvu pamoja na FARDC ili ya kutafuta amani huko.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire