Kinshasa : Korti kuu ya katiba imechukuwa hatua ya kumurudisha madarakani liwali Théo Ngwabidje KASI

Korti kuu ya katiba nchini DRC imemurudisha madarakani liwali wa jimboni la Kivu ya kusini Théo Ngwabidje KASI.

Hii kutokana na azimio ya korti hiyo iliyo tangazwa tangu ma juzi mjini Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Ni kwa ombi lake liwali Ngwabidje akipinga hatua ya bunge la jimbo ya Kivu ya kusini ya tarehe 2 disemba 2021.

Jean Claude MUBALAMA kiongozi wa ofisi ya kazi ya liwali ndiye alihakikisha kwenyi vyombo vya habari nchini DRC habari hii.

Tufahamishe kwamba ni sasa miezi Kadhaa jimbo la Kivu ya kusini laongozwa naye liwali makamu tangu baada ya vuta ni kuvute iliyojitokeza kati ya wabunge kadhaa wa jimbo na serkali yake Théo Ngwabidje KASI.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire