Vijana wa eneo za Kasindi Lubiria mpakani mwa nchi ya Uganda tarafani Beni zaidi ya arubaini wamekubali kutumikia nchi kwa kujiorodhesha ndani ya jeshi la taifa FARDC. Hawa walikula kiapo mbele ya bendera ya taifa kutumikia nchi maishani mwao.
Akizungumza kwenyi vyombo vya habari, Luteni PUNA akiwa kamanda wa uongozi wa jeshi pa Kasindi aangazia kwamba vijana hawa wamefanya chaguo nzuri.
Huyu aunga wazazi mkono ambao waliweza kuwahamasisha kufanya kazi hiyo nzuri, kwani yanalenga kutetea nchi.
Upande wa vijana husika, hawa wanena kuamua wenyewe bila mkazo wowote ule. Wakipenda kusaidia DRC ili kukomesha usalama mdogo kila leo na kutekeleza amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo waeleza wamoja miongoni mwa vijana hawo.
Wengine wengi wasisitiza kwamba kuna faida kubwa mtu kuchukuwa hatua ya kutumikia nchi yake, hii yamaanisha upendo kwake.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.