Kivu ya kusini/ Kabare: MONUSCO ajielekeza huko kutafuta suluhu kuhusu shida ya wakaazi

Kabare ya kaskazini

Wakaazi wa Luhihi wilayani Kabare wanena kutendewa ukiukaji wa haki ya binaadam na maadui wa amani. Ni kutokana na usalama mdogo unaotanda siku hizi eneo hilo.

Waliweza kutamka hayo juma tano tarehe 9 februari 2022, wakati wa mkutano na MONUSCO pamoja na mashirika za usalama jimboni Kivu ya kusini.

Shirika hii la umoja wa kimataifa lilijielekeza pa Luhihi kujionea gisi hali ya usalama ilioko, pamoja na hayo kutafuta suluhu ya pamoja.

Wakati huo miungano za shirika la raia zilipata fursa ya kutoa shida zinazo wakumba ili kutafuta suluhisho. Akiweko Administrera wa wilaya ya Kabare.

Upande mwengine bondeni Ruzizi pa Kamanyola wilayani Walungu, hali ya usalama yafanana kuwa shwari. Duru toka huko zaeleza kuwa matokeo hayo ni nguvu za pamoja MONUSCO na Jeshi la taifa FARDC. Wakaazi hawa waomba viongozi kuzidisha nguvu ili kurejesha usalama eneo hilo la wilaya ya Walungu.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire