Kinshasa : Miili ya wahanga wa ajali ya moto wa umeme itapelekwa kwenyi makao yao ya mwisho

Miili ishirini na tano ya wahanga wa ajali ya nguvu za umeme itapelekwa kwenyi makao ya mwisho huko tu mjini Kinshasa. Ni hii ijumaa tarehe 11 februari 2022, ndipo sherehe za kusindikiza miili hiyo ya wahanga wa ajali iliyojitokeza kwenyi soko Matadi Kibala itafanyika.

Ripoti toka mjini Kinshasa zanena kuwa maandalizi kuhusu sherehe za mazishi ilifanyika kwenyi Hôtel de ville mjini Kinshasa.

Ni kwa uongozi wake waziri jimboni husika na swala za kijamii kwa ushirikiano ya wanamemba wa serkali jimboni humo.

Kutokana tu na duru zetu , baada ya kufikiri kuhusu kazi zitakazo tekelezwa na ni katika hali gani, walikusudia mazishi ifanyike hii ijumaa tarehe 11 februari 2022.

Tukumbushe kuwa kwa jumla ni miili ya watu ishirini na tano ndio itawekwa ndani ya udongo. Ajali iliyosababishwa na nguvu za moto wa umeme toka singa kubwa baada ya mvua kunyesha.

Wahanga walikutwa sokoni asubui katika shuguli zao za byashara kama ilivyo desturi wakati walipatwa na vifo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire