Goma : François Masumbuko RUBOTA akuja kucunguza kazi katika sekta ya maendeleo vijijini

François Masumbuko RUBOTA waziri husika na maendeleo vijijini nchini DRC.

Waziri husika na maendeleo vijijini François Masumbuko RUBOTA yupo ziarani mjini Goma tangu ijumaa tarehe 11 februari 2022, akijielekeza pia mjini Bukavu jimboni Kivu ya kusini.

Waziri François Masumbuko RUBOTA akuja kucunguza namna kazi zatekelezwa katika sekta ya maendeleo ambayo anayoiongoza nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

Kwenyi uwanja wa ndege pa Goma, alipokelewa kwa shangwe na vigelegele na umati wengi miongoni wafwasi wa chama chake cha kisiasa MSR.

Wafwasi wa chama cha kisiasa MSR

Alipokelewa pia na viongozi kadhaa wa MSR jimboni Kivu ya kaskazini pamoja naye Jenerali Sylvain Ekenge akiwakilisha liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini.

François Masumbuko RUBOTA akiomba raia kuwa waaminifu kwake Raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI ambaye hupiganisha kila leo ili kirejesha usalama mashariki mwa nchi.

Baada ya uwanja wa ndege, waziri husika na maendeleo vijijini asindikizwa na mlolongo wa gari hadi kwenyi jumba la mapokezi LINDA mjini Goma. Pâle alibaki saa chache kabla ya kwenda muona liwali wa jimbo, kuhusu lengo la ziara yake.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire