Katika ujumbe wake kwa serkali ya DRC na hata kwa mashirika zisizo za kiserkali, mtetezi wa haki ya wana Rutshuru, moja wa viongozi huko Aimé Mukanda Mbusa afanya utetezi kuhusu hali mbovu ya barabara zenyi kuunganisha vijiji vilivyo kumbwa na usalama mdogo. Barabara hizo ziweze kujengwa.
Akitaja mfano barabara ya Binza, usultani wa Bwisha, barabara Kisharo, Kihito, Kasave, Nyabanira, Ngenda. Barabara yenyi umbali wa kilomita zaidi nne, ikifaidia kwa raia zaidi ya thelasini na tatu elfu.
Bwana Aimé Mukanda aongeza kuwa barabara hiyo ni njia moja wapo ya kurahisishia wakaaji kupeleka mimea ya shamba kwenyi soko kubwa.
Huyu ataja pia barabara Kamukwale, Sarambwe, Nyarubogo, Kanyabayonga, barabara Nyamilima, Nyabitale, Nyamitwitwi, Busera, Kitwiguru na zinginezo.
Kiongozi huyu akumbusha kwamba asilimia tisini na tano raia wa Rutshuru waishi kupitia kilimo. Akiongeza kwamba kufunguliwa kwa barabara hizo kutarahisishia walinzi wa usalama kuwagonga makundi zenyi kumiliki silaha wa mahali na wa ugenini. Pamoja na hayo kupunguka kwa njaa.
Kwa ukumbusho ni miaka 28 sasa tangu raia wilayani Rutshuru waishi hali mbovu. Vijiji kuchomwa moto, raia kuyahama maskani, vijiji kuvamiwa na kundi zenyi kumiliki silaha za mahali na za kigeni.
Chumba cha wandishi
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.