Kivu ya kusini : Wakaaji wengi walia njaa bondeni Ruzizi kutokana na mazao mabaya ya shamba

Kiliba ONDS bondeni Ruzizi

Wakaazi bondeni Ruzizi watao malalamiko kuhusu ukosefu wa chakula siku hizi. Hali yenyi kusababisha njaa na watoto wengi kutoenda shuleni , wakikosa pia malipo ya shule hasa kwa wale wa shule za sekondari.

Wakaazi hawa wanena kwamba hayo yatokana na mavuno mabaya yao kwa kipindi kilicho pita.

Mkaaji moja toka bonde la Ruzizi akihojiwa kwa vyombo vya habari ajulisha kuwa Wakaaji wategemea kilimo eneo hilo. ndio ya sababu ya hali ya maisha kukwama maana hawana msaada mwengine.

Shingiri Binda jina la mkaazi aomba serkali pamoja na wafadhili wake kujihusisha na jambo hilo. Akiomba kuhimiza wakaazi kuwa na gala ambamo watachunga sehemu ya mazao ya shamba.

Huyu aongeza kuwa hatua hiyo itarahisisha kwa kila jamaa kutuma mwanafunzi shuleni baada ya kutumia chakula. Duru hunena kwamba ukosefu wa mvua ndio ilipelekea ukosefu wa mazao ya shamba.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire