Habari toka jimboni Kivu ya kusini ni kwamba ndege moja ya shirika AGEFRECO imewaka moto. Ilikuwa ikitoka Kavumu na kujielekeza pa Lulingu. Dakika chache kiisha kuondoka ilirudi Kavumu ikiwaka moto.
Duru za mahali hunena kwamba ndege hiyo ilikuwa ikiendesha kazi ya byashara, wakati ilipatwa na ajali.
Ni hii juma tatu tarehe 14 januari 2022 majira ya saa kumi za jioni . Hadi sasa hakuna mtu aliyefariki dunia. Ndege yenyewe kuteketea kwa moto.
Duru zingine zafahamisha kwamba ni mara ya tatu ndege hiyo kupatwa na ajali na hiyo yatokana na uzembe kwa wenyeji kutotengeneza chombo hicho kinacho hatarisha maisha ya raia.
Juvénal Murhula.
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.