Goma: Wasichana wenyi umri chini ya miaka 16 wa Shule Uwezo ya mji wameshukuru kwa juhudi za liwali wa jimbo kabla ya kujielekeza kwenyi michuano ya kandanda barani Afrika mjini Kinshasa

.

Liwali wa jimbo la Kivu ya kaskazini Luteni Jenerali Constant Ndima Kogba

Wasichana hawa wenyi umri wa miaka chini ya 16 wa shule Uwezo la CEPAC walisindikizwa na viongozi wao wa shule, walishukuru liwali kuwasindikiza katika michezo ya kandanda hadi kuchukuwa nafasi ya kwanza mjini Kinshasa. Ilikuwa fursa ya kumuonyesha liwali zawadi waliopewa baada ya ushindi.

Viongozi wao wanena kwamba wasichana hawo wata wakilisha DRC kwenyi mashindano ya kandanda barani Afrika ambayo itaanza tarehe 19 februari 2022, na kwamba watajielekeza mjini Kinshasa tarehe 17 februari 2022 ajili ya michuano.

Liwali wa jimbo aliendelea kuahidi kuwaunga mkono ili wafaulu kwa michuano ya Afrika itakayopelekea hiyo ya barani.

Chumba cha wandishi

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire