Ubeljiji: DRC yashiriki kwenyi kilele kinacho fanyika Brussels kikikusanya Muungano wa Ulaya pamoja na Afrika

Brussels/ Ubeljiji

Kumefunguliwa hii alhamisi tarehe 17 februari huko Brussels kilele cha kumi na sita kati Muungano wa Ulaya pamoja na wa Afrika. Mkutano mkuu ambao waziri mkuu Sama Lukonde awakilisha raisi wa DRC Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO.

Muda wa siku mbili washiriki kilele watazungumza kuhusu uhusiano kati ya Ulaya na Afrika. Kikao hicho kitakusanya vikundi tano kuhusu mada tano tofauti.

Yaani Amani, usalama, uongozi, mambo ya afya na kutoa chanjo, kilimo na maendeleo, maadibisho, utamaduni na mafunzo kuhusu chanjo, sekta ya kipekee na uchumi, kubadilika kwa mazingira na umeme, ujenzi, technologia nyipya , kuinuka kipesa pamoja na kadhalika.

Kabla ya kikao kuanza, waziri mkuu alitembelea jumba la kiutamaduni la Brussels akiweko mwenziwe wa Ubeljiji Alexandre Decrou.

Sama Lukonde ametazama utajiri uliomo ndani ya jumba hilo ambao ni mali kutoka DRC. Waziri asema kufurahi kwani utajiri huo wabaki ndani ya historia ya Ubeljiji na DRC.

Waziri mkuu toka Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo anena kwamba kikao hicho ni mhimu kwa DRC ambayo yahitaji amani na usalama.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire