Kivu ya kaskazini/ Nyiragongo : Watetezi wamoja wa haki za binaadam wa Rusayo walazimisha kufunguliwa kwa wakaazi wasio na hatia wa Kijiji Kabale Katambi

Watu wa Nyiragongo

Ukiukaji wa sheria waripotiwa kwenyi Kijiji Kabale Katambi wilayani Nyiragongo. Watatu wa Kijiji hicho wakiwa korokoroni walifungwa na taasisi za sheria.

Kwa hiyo watetezi wa haki ya binaadam pa Rusayo waomba waachiliwe huru watu hawo wanaofungwa kwenyi jela kuu Munzenze bila hatia yoyote.

Wakizungumza kwa njia ya simu kwenyi vyombo vya habari, wanena kwamba wahanga ni wakaazi wawili wa eneo hilo la mtaa wa Nyiragongo ndio walishikwa tarehe 11 februari na mwengine tarehe 13 februari. Wote walipelekwa ndani ya jela Munzenze tarehe 15 februari 2022.

Wahanga washutumiwa kuwaswali watu waliotumwa ndani ya Kijiji chao kupima viwanja bila wenyeji kuweko.

Watetezi hawa waomba viongozi wa sheria kutafuta suluhu kwa swala hilo maana makubaliano kimagendo kuhusu viwanja eneo hilo ni chungu tele.

Chumba cha wandishi.

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire