Kivu ya kusini/ Kamituga: Hali ya maisha yazorota kupitia barabara mbovu Bukavu Mwenga ikiomba ujenzi wa serkali

Jumba la mea wa mjini Kamituga

Mea wa mji wa Kamituga Ngila Butia Alexandre aomba serkali jimboni na kwenyi ngazi za taifa kujihusisha katika ujenzi wa barabara Bukavu Mwenga. Hali mbovu ya barabara yapelekea kupandishwa kwa bidhaa mjini Kamituga.

Hayo yalikusudiwa katiba shauri ya usalama mjini Kamituga wilayani Mwenga wiki hii ikiongozwa naye mea mwenyewe.

Akieleza kwamba raia wasumbuka kutokana na hali mbovu ya barabara hiyo, kabla kuwasili mjini Bukavu ama Kamituga wilayani Mwenga. Wengi wachukuwa pikipiki jambo ambalo lasababisha kupandishwa kwa bei ya bidhaa yaani chakula na vifaa vingine vya samani.

Mea wa mji aligusia pia vilalo vingi kwenyi barabara hiyo katika hali mbovu ambavyo vyastahili ujenzi wa serkali.

Kwa kungojea msaada kwa serkali Ngila Butia Alexandre anena kuwa mkutano mwengine unaandaliwa hapa karibuni ili kujaribu kutafuta suluhu kwa kungojea serkali. Kikao hicho kitajumwisha watumiaji wa barabara yaani wenyeji lori na wengineo.

Juvénal Murhula

Soyez le premier à commenter

Poster un Commentaire