Siku hizi mashaka yaendelea kutawala mioyo ya raia walio wengi nchini kuhusu ujio wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, kutokana na hali waishimo. Wengine huwa na matamaini kwamba watayaona mabadiliko kupitia ahadi zake raisi wa nchi Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO.
Ijapo juhudi zake katika kutaka kutekeleza amani mashariki mwa nchi, vitendo vya ugaidi kila leo mjini kama vijijini ni chungu tele hususan mashariki mwa DRC. Pamoja na hayo kusoma bure kwa watoto wa shule za msinji ijapo kuna shule na hata walimu ambao hadi sasa wangojea walipwe mishahara na serkali.
Kupiganisha rushwa katika sekta mbalimbali za nchi ili kuinua uchumi na hiyo itakuwa moja wapo kujibu kijamii kwa maisha ya raia. Ijapo wanyanyasi wamoja waendelea kuinua vichwa, hawajapigwa fimbo.
Upande wa kidiplomasia safari sisizo na hesabu zake Raisi ili ya uhusiano bora na nchi jirani pamoja na zingine za kimataifa katika kuisaka amani n’a maendeleo ya nchi.
Ijapo wengine huzani kwamba safari hizo zapita kiasi na kwamba zahatarisha mali ya nchi kipesa, hayo na mengineo.
Watalaam nawo hujiswali, kipi kitachoboresha hali ya maisha nchini DRC ingawa utawala utaonekana kuwa ni mzunguko ya wenyewe kwa wenyewe. Nani Musa wa DRC aje akaiokowe, kwa kuwa imefananishwa na lori ambayo imekwama shimoni ikihitaji msaada. Wanao nia nzuri kwa kuiokowa ni wachache ila wengi hujikatia vipande kama vile nyama ya tembo.
Kwa ukumbusho uchaguzi wa kidemokrasia, huru na wazi ulianza nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo mwaka 2006, migogoro hujitokeza kila leo miongoni mwa wagombea. Mwaka huo ilikuwa vuta nikuvute kati yake Raisi wa zamani Joseph Kabila Kabange naye Raisi makamu wa zamani Jean Pierre Bemba Gombo.
Joseph Kabila Kabange akachukuwa utawala muda wa miaka kumi na munane.
Wadadisi wa mambo kadhaa hunena kwamba nukta mhimu aliyofaulu Joseph Kabila wakati wa utawala ni kuweza kuunganisha nchi ambayo ilitaka kugawanyika. Ijapo hali mbovu ya maisha na uchumi kukwama.
Halafu uchaguzi mwaka 2011 ulionekana tishio kubwa. Migogoro ilizuka kati ya wagombea tangu kampeni ya uchaguzi hadi matokeo yake. Wagombea wakitowa kauli kuibwa sauti. Joseph Kabila mara tena kachukuwa utawala iliyopingwa naye ayati Étienne TSHISEKEDI aliyejitangaza binafsi nyumbani kwake kwamba ni yeye mshindi. Baadae hali ya maisha yaliendelea kuzorota yaani usalama mdogo mashariki mwa DRC, hali kukwama kijamii na kiuchumi. Huku raia wakilia aache madaraka Joseph Kabila Kabange.
Kipindi cha tatu mwaka 2018, wagombea miongoni mwao Emmanuel Shadari upande wa raisi Joseph Kabila alieondoka madarakani kwa kutoruhusiwa mara tena na katiba. Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO wa chama UDPS na Martin FAYULU wa chama LAMUKA.
Baada ya uchaguzi, kila moja alikuwa akishuhudiya ushindi. Wengi kushangaa Tume huru ya uchaguzi kumtaja Félix Antoine TSHISEKEDI TSHILOMBO aliye madarakani leo kuwa ni yeye alifaulu kiti cha uraisi. Jambo lilimshituwa moyo Martin FAYULU na wafwasi wake wakati huo.
Wakizania muda wa siku nyingi kama kutakuwa na mabadiliko mengine ijapo matokeo yalikuwa imetangazwa kisheria.
Juvénal Murhula
Poster un Commentaire
Vous devez vous connecter pour publier un commentaire.